MADRID.Mahakama kuu yawazuia wagombea kusimama katika uchaguzi wa serikali za mitaa | Habari za Ulimwengu | DW | 06.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MADRID.Mahakama kuu yawazuia wagombea kusimama katika uchaguzi wa serikali za mitaa

Mahakama kuu ya Uhispania imewazuia mamia ya wagombea kusimama katika uchaguzi wa serikali za mitaa katika jimbo la kaskazini la Basque.

Wagombea hao wamedaiwa kuhusika na kundi lililopigwa marufuku la chama cha Batasuna.

Mahakama hiyo imepitisha uamuzi kwamba kundi la kisosholisti la Aberzale linaunga mkono juhudi za tawi la kundi la kisiasa linalopigania kujitenga kwa jimbo la Basque la ETA.

Kundi la ETA kwa zaidi ya miaka 30 limekuwa likiendesha kampeini za kupigania uhuru wa jimbo la Basque kaskazini mwa Uhispania na kusini magharibi mwa Ufaransa na kusababisha kuuwawa kwa zaidi ya watu 800.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com