Maafisa 7 wa polisi wauwawa | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 01.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

IDHAA YA KISWAHILI

Maafisa 7 wa polisi wauwawa

---

RAMPUR INDIA

Maafisa saba wa polisi na raia mmoja wameuwawa katika mashambulizi yaliyofanywa na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wakiislamu katika kambi moja ya polisi kaskazini mwa India kwenye jimbo la Uttar Pradesh.

Duru za kiuslama zimesema kwamba watu waliokuwa na bunduki walipambana na polisi walipojaribu kuingia kambi hiyo ya polisi ya Rampur.Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na uvamizi huo ingawa kituo kimoja cha matangazo katika eneo hilo kimenukulu duru za wizara ya mambo ya ndani zikisema wanashuku uvamizi huo umefanywa na kundi la wanamgambo wa kiislamu la Lashkar e Taiba.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com