LUSAKA:Mzigo wa kasuku wanaswa uwanja wa kimataifa wa Lusaka | Habari za Ulimwengu | DW | 24.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LUSAKA:Mzigo wa kasuku wanaswa uwanja wa kimataifa wa Lusaka

Maafisa wa serikali nchini Zambia wanazuia mzigo ulio na zaidi ya ndege 200 aina ya kasuku waliopangwa kusafirishwa hadi Singapore.Kwa mujibu wa afisa wa serikali ndege hao hawakuwa na hati za sawasawa za usafirishaji.

Mzigo huo wa aina tofauti za kasuku ulikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Lusaka wiki jana na Halmashauri ya Wanyama wa Porini ya Zambia ZAWA kulingana na msemaji wake Maureen Mwape.

Kwa mujibu wa Bi Mwape msafirishaji wa ndege hao hakuonyesha hati zilizohitajika kama inavyolazimu sheria ya kimataifa kuhusu wanyama walio na hatari ya kuadimika CITES.Bi Mwape anaongeza kuwa walilazimika kuwarejesha ndege hao nchini Guniea ambako walitokea.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com