LONDON:Zimbabwe yapewa mkopo na Benki za Uingereza | Habari za Ulimwengu | DW | 29.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON:Zimbabwe yapewa mkopo na Benki za Uingereza

Kampuni tatu za Uingereza ikiwemo Benki ya Barclays zinaipa nchi ya Zimbabwe msaada wa fedha mkubwa.Kulingana na gazeti la The Observer Benki ya Standered Chartered na kampuni ya Bima ya Old Mutual zinaripotiwa kuunga mkono nchi hiyo iliyo na utawala unaokiuka haki za binadamu kwa mujibu wa mashirika ya kutetea haki za binadamu ulimwenguni.

Kulingana na uchunguzi uliofanywa na gazeti la Africa Confidential ,Benki ya Barclays inaipa kampuni moja ya serikali ya Zimbabwe mkopo wa euro milioni 46 ili kuimarisha mpango wa marekebisho ya umiliki wa ardhi.

Sera hiyo ya Rais Mugabe iliyosababisha tetesi ilipelekea serikali kunyakua mashamba alfu 4 ya wakulima walio na asili ya Wazungu na kugawanyiwa wakulima wa asili ya Afrika waliokuwa hawana mashamba.

Kulingana na gazeti hilo kampuni hizo tatu zinaipa serikali ya Mugabe msaada wa zaidi ya euro bilioni moja.Kwa mujibu wa msemaji wa benki ya Barclays nchini Zimbabwe kampuni hiyo inaendelea kutoa huduma kwa wateja wanaokabiliwa na mazingira magumu ya kibiashara.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com