1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London.Msaada wa pamoja kuhusu wahamiaji wajadiliwa huko Uingereza.

26 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCz4

Mawaziri wa mambo ya ndani kutoka nchi sita kubwa za Umoja wa Ulaya, wanakutana mjini Stratford-upon-Avon, Uingereza kujadili kuungana pamoja katika sera za uhalifu na uhamiaji.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble na waziri mwenziwe wa Ufaransa Nicolas Sarkozy wanatarajiwa kutia kishindo juu ya kuundwa kwa sera za pamoja za uhamiaji.

Sera hii itakuwa na maana ya kuunda sera moja ya Umoja wa Ulaya ya hifadhi ya wakimbizi na kufungua soko la wafanyakazi katika nchi za Umoja huo kwa wafanyakazi wageni wa muda.

Mawaziri wa mambo ya ndani wa Uingereza, Uhispania, Italy na Poland pia watahudhuria katika mkutano huo wa siku mbili, ulioanza jana kwa majadiliano ya kuweka sera ya pamoja ya kupambana na ugaidi.