LONDON: Watu 2 wengine wakutikana na chembe za sumu | Habari za Ulimwengu | DW | 02.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON: Watu 2 wengine wakutikana na chembe za sumu

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier

Kufuatia kifo cha jasusi wa zamani wa Kirussi Alexander Litvinenko,sasa msomi wa Kitaliana, Mario Scaramella aliewasiliana na Litvinenko amekutikana na chembe za mnururisho baada ya kuchunguzwa na wanasayansi wa Kingereza. Scaramella alie mtaalamu wa upelelezi,alikutana na Litvinenko katika mkahawa mmoja mjini London, muda mfupi kabla ya Litvinenko kuanza kuugua na baadae kufariki hospitalini kwa sababu ya sumu ya chembe za mnunurisho za Polonium 210.Litvinenko aliekuwa mkosoaji mkali wa rais Vladimir Putin wa Urussi,alikuwa akichunguza mauaji ya muandishi wa habari wa Kirussi Anna Politkovskaya.Wakati huo huo,waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza John Reid amesema,mmoja katika familia ya Litvinenko pia amekutikana na chembe za mnururisho.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com