LONDON: Naibu waziri mkuu wa Irak, Barham Saleh, yuko ziarani nchini Uingereza | Habari za Ulimwengu | DW | 23.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON: Naibu waziri mkuu wa Irak, Barham Saleh, yuko ziarani nchini Uingereza

Naibu waziri mkuu wa Irak Barham Saleh anaifanya ziara nchini Uingereza na tayari amepokewa kwa mazungumzo na waziri mkuu Tony Blair.

Katika mazungumzo na waandishi wa habari, Barham Saleh, amekataa kuzungumzia juu ya matamshi ya mwanadiplomasia moja wa Marekani kwenye televisheni ya kiarabu ya Al-Jazeera mwishoni mwa wiki kwamba sera za Marekani nchini Irak zinaonyesha kiburi na ujinga. Mwanadiplomasia huyo, Alberto Fernandez, baadae alijirekebisha na kusema ulimi ulikuwa umeteleza.

Akiielezea hali ilivyo kwa jumla nchini Irak, Barham Saleh amesema swala la Irak ni la kushughulikia kwa makini:

´´Lazima tushughulike tukizingatia kuwa kuna dharua. Dharua kubwa ila tusiwe na wasi wasi. Tunahitaji kuzingatia hali halisi ya mambo lakini tusijiuzulu. Tumekuwa tukijaribu kuimarisha idara zetu za usalama na utaratibu wa kidemokrasia wa kisiasa wakati tukikabiliana na vita vya kimataifa dhidi ya ugaidi. Irak ni sehemu ya eneo zima´´.

Akiulizwa kuhusu uwezekano wa mpango wa kuyaondoa majeshi ya kigeni kutoka Irak, naibu waziri mkuu wa Irak, Barham Saleh, amesema Irak inatumai kuongoza kijeshi karibu nusu ya mikoa kabla ya mwaka huu kumalizika.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com