LONDON: Mpelezi wa zamani wa Rushia, afariki dunia kwa sumu | Habari za Ulimwengu | DW | 24.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON: Mpelezi wa zamani wa Rushia, afariki dunia kwa sumu

Mpelelezi wa zamni wa Rushia, Alexander Litvinenko amefariki dunia. Litvinenko mwenye umri wa miaka 41, alikuwa akitibiwa katika hospitali mjini London nchini Uingereza, kwa kile kilichodhaniwa alipewa sumu.

Rafiki moja wa Litvinenko amesema, mnamo majira ya usiku, alikuwa akikabiliwa na matatizo ya moyo na kusaidiwa na mashine. Taarifa za vyombo vya habari zimesema madaktari waliokuwa wakimshughulikia, wamegundua vitu vitatu vya maajabu tumboni mwake.

Litivinenko alisema alianza kujisikia kuumwa baada ya mkutano na raia wawili kutoka Rushia kwenye hoteli tarehe 1 mwezi huu.

Haijajulikana ni sumu gani iliotumiwa lakini wataalamu wa maswala ya sumu wanadhani kuwa sumu aina ya Thallium ndio ilitumika.

Alexander Litvinenko alikuwa ni mtu asiyeogopa kusema ukweli na alikuwa akifanya uchunguzi juu ya mauaji ya mwanahabari wa Rushia, bibi Anna Politkovskaya. Aliishutumu serikali ya Rushia kuhusika na matukio yote hayo mawili.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com