1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Mawaziri wa kigeni wa baraza la usalama wakutana leo

6 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5h

Mawaziri wa mashauri ya kigeni wa nchi tano wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, wanakutana leo mjini London Uingereza kujadili athari zitakazotokea kuhusuiana na mpango wa nyuklia wa Iran.

Marekani ikiungwa mkono na Uingereza, inataka Iran iwekewe vikwazo lakini China na Urusi zinapinga hatua hiyo.

Mkutano huo unafanyika baada ya kiongozi anayehusika na mashauri ya kigeni wa Umoja wa Ulaya, Javier Solana, kujaribu kuishawishi Iran iachane na mpango wake wa kinyuklia.