LONDON: mabadiliko ya hali ya hewa yatishia juhudi za kuondoa umasikini barani Afrika | Habari za Ulimwengu | DW | 29.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON: mabadiliko ya hali ya hewa yatishia juhudi za kuondoa umasikini barani Afrika

Wawakilshi wa mashirika ya mazingira na maendeleo wamesema kwamba bara la Afrika linakabiliwa na maafa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na huenda hali hiyo ikavuruga juhudi za kuondoa umasikini.

Wawakilishi hao wamesema mjini London ,kuwa hatua za haraka lazima zichukuliwe na jumuiya ya kimataifa .

Mkuu wa utafiti kwenye shirika la misaada, Oxfam Duncan Green amesema kwamba mabadiliko hayo ya hali ya hewa yanayotokea barani afrika yanawaathiri hasa watu masikini. Bwana Green ameeleza kuwa athari hizo ni pamoja na mafuriko, ukame na vimbunga.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com