LOME:Uchaguzi wa wabunge wafanyika hii leo upinzani washiriki | Habari za Ulimwengu | DW | 14.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LOME:Uchaguzi wa wabunge wafanyika hii leo upinzani washiriki

Raia wa Togo wanapiga kura hii leo katika uchaguzi wa wabunge ambako vyama vyote vikuu vya kisiasa vinawakilishwa.Hii ni mara ya kwanza baada kususia uchaguzi kwa zaidi ya miongo 2 kwa chama cha Olympio UFC kinawania nafasi na kutaka kukiondoa chama tawala cha Rally of Togolese People, RPT.

Uchaguzi huo unalenga kutathmini madaraka ya chama tawala aidha iwapo taiafa hilo litapata msadaa kutoka kwa Umoja wa Ulaya baada ya kusitisha kwa kipindi cha miaka 14.

Umoja wa Ulaya kwa upande wake unashinikiza kufanyika kwa uchaguzi unaotimiza itifaki za kisiasa zilizoafikiwa katika mazungumzo ya kina.Kundi kubwa la waangalizi tayri limeshawasili nchini humo ili kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unakuwa wa huru na haki.

Takriban wapiga kura milioni 3 wanatarajiwa kushiriki katika shughuli hiyo itakayoendelea kutwa nzima katika yapata vituo 5900 vya kupigia kura.

Jumla ya wagombea 2199 wa binafsi wanaowakilisha vyama 32 vya kisiasa wanawania viti 81.Maafisa wa usalama walipiga kura alhamisi iliyopita ili kuwapa nafasi kusimamia wapiga kura hii leo.

Chama tawala cha RPT kinajipigia debe kwa kueleza mafanikio yake tangu Rais Faure Gnassingbe kuwa madarakani kwa kipindi cha miaka 2.Bwana Gnassingbe aliteuliwa na jeshi na kuingia madarakani mwaka 2005 kufuatia kifo cha babake Gnassingbe Eyadema.Kiongozi huyo kijana alijiuzulu na kushinda uchaguzi baada ya miezi miwili uliosusiwa na vyama vya upinzani.Umoja wa Ulaya kwa upande wake unashikilia kuwa sharti kila mpiga kura aliyesajiliwa anapata haki ya kumchagua mgombea atakaye ndipo Togo ipokee msaada baada ya kusitishwa kwa miaka 14.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com