LISBON:Ureno kuzingatia zaidi suala la Ulinzi katika Umoja wa Ulaya | Habari za Ulimwengu | DW | 26.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LISBON:Ureno kuzingatia zaidi suala la Ulinzi katika Umoja wa Ulaya

Waziri wa ulinzi wa Ureno amesema nchi yake ambayo kwa sasa inashikilia uwenyekiti wa kupokezana wa Umoja wa Ulaya inataka suala la Ulinzi kuwa muhimu zaidi katika Umoja huo. Kwa mujibu wa gazeti la Gurdian Nuno Severiano Teixeira amesema uwezo wa kijeshi ni muhimu katika kuimarisha uhusiano katika eneo la Ulaya na Marekani na pia kuimarisha usalama duniani na kwenye Umoja huo.

Aidha amesema uwezo wa kukabiliana na hali ya mizozo unahitaji kuimarishwa kupitia uimarishaji wa nyezo za ardhini angani na baharini miongoni mwa masuala mengine.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com