1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Libya-Baraza la Usalama

Oumilkher Hamidou27 Februari 2011

Shinikizo linazidi kuwa kubwa dhidi ya kiongozi wa mapinduzi ya Libya Muammar Gaddafi na jamaa zake kwa kuziendeya kinyume haki za binaadam.

https://p.dw.com/p/10QEA
Muammar GaddafiPicha: picture alliance/dpa

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limepitisha kwa sauti moja hatua dhidi ya kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi na jamaa zake.Vikwazo hivyo vinaanzia marufiku ya silaha,kusafiri na kufungwa akaunti zao.Taasisi hiyo muhimu ya Umoja wa Mataifa imefungua njia pia ya kuweza kuandamwa pengine Gaddafi na jamaa zake mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mjini The Hague kutokana na matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji wanaoipinga serikali nchini Libya.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaituhumu serikali ya mjini Tripoli kukiuka haki za binaadam.Katika maeneo yaliyokombolewa ya Libya,upande wa upinzani unaanza kujiandaa. Waziri wa zamani wa sheria Mustafa Abdul Ashleyl ametangaza kuundwa serikali ya mpito ambayo wanachama wake watatokea katika maeneo yote ya nchi hiyo.Benghazi ndio yatakayokua makao makuu ya serikali hiyo ya mpito-hadi Tripoli utakapokombolewa anasema waziri huyo wa zamani wa serikali ya Gaddafi.Kituo cha televisheni cha Al Djazira kimeripoti kwamba vikosi tiifu kwa Gaddafi vinaendelea kudhibiti sehemu kubwa ya Tripoli.