LEXEMBOURG Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wajadili bajeti mjini Luxembourg | Habari za Ulimwengu | DW | 13.06.2005
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

LEXEMBOURG Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wajadili bajeti mjini Luxembourg

Mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka mataifa ya jumuiya ya Ulaya wanakutana huko Lexembourg. Mazungumzo yao yanalenga kuondoa tofauti za mataifa yao kuhusiana na bajeti ya jumuiya hiyo ya mwaka wa 2007 hadi 2013. Swala tete ni kiwango cha pesa Uingereza inachopokea kila mwaka kutoka kwa umoja wa Ulaya kwa kulipa fedha taslimu.

Kabla mkutano huo kuanza, rais wa halmashauri ya jumuiya ya Ulaya, Jose Manuel Barroso, alimtolea wito waziri mkuu ya Uingereza bwana Tony Blair, kukiwachilia kiwango hicho. Lakini kufikia sasa Uingereza haina mpango wa kulikubali ombi hilo.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza, bwana Jack Straw, aliwaambia waandishi habari mda mfupi baada ya kuwasili mjini Luxemboug kwamba Uingereza itatumia kura yake ya turufu kuilinda haki yake ya kuendelea kupokea kiwango hicho cha fedha. Uingereza ilianza kupokea fedha hizo mwaka wa 1984 kufuatia majadiliano makali yaliyoongozwa na aliyekuwa waziri mkuu wakati huo, Bi Margaret Thatcher.