Kundi la Wasunni lajiondoa bungeni. | Habari za Ulimwengu | DW | 02.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kundi la Wasunni lajiondoa bungeni.

Baghdad.Kundi muhimu la wasunni nchini Iraq limejiondoa kutoka katika bunge wakipinga kile kinachodaiwa kuwa ni kuwekwa jela kwa kiongozi wao Adnan al-Dulaimi. Kiongozi huyo wa chama cha Sunni Front Party amewekwa chini ya ulinzi nyumbani kwake. Mtoto wake na wanachama wengine kadha katika ujumbe wake pia wamekamatwa. Msemaji wa kundi hilo amesema kuwa halitarejea bungeni hadi pale Adnan al-Dulaimi atakaporuhusiwa kutoka nyumbani kwake. Mkwamo huo unatishia kuongeza wasi wasi baina ya madhehebu kati ya serikali inayoongozwa na Washia waliowengi na Wasunni Waarabu ambao ni wachache.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com