Kombe la UEFA | Michezo | DW | 06.12.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Kombe la UEFA

Hamburg na Everton zakata tiketi za duru ijayo ya kombe la UEFA.

default

Hamburger SV

Katika kinyan’ganyiro cha jana cha kombe la UEFA-kombe la shirikisho la dimba la ulaya,Hamburg ya Ujerumani na Everton ya Uingereza ,ni miongoni mwa timu zilizokata tiketi zao kwa duru ijayo ya timu 32 zilizosalia.

Mabingwa wa Ulaya AC Milan, wakiongozwa na stadi wa Brazil,Kaka,wamewasili Tokyo, Japan kwa kinyan’ganyiro cha kombe la dunia la klabu bingwa.

Na Didier Drogba,stadi wa Chelsea, anahitaji opreshini ya goti.Je,stadi huyo wa Ivory Coast atalikosa kombe la Afrika la mataifa nchini Ghana mwezi ujao ?

Bao la dakika za mwisho alilipachika Tim Cahill liliikatia Everton ya Uingereza tiketi ya duru ijayo na kuiacha nyuma Zenit St.Petersberg ya Urusi.Nigel de Jong na piotr Trochowski wamelifumania lango la Dinamo Zagreb na kuikatia Hamburg ya Ujerumani tiketi yao ya duru ijayo ya kombe la UEFA.Mabingwa wa kombe la taifa la ujerumani Nüremberg waliokoa matumaini yao ya kujiunga na hamburg duru ijayo kwa kuizaba Alkmaar ya Holland mabao 2:1.Alikua staid wao Marek Mintal alietamba.Lakini ilikua Alkmaar iliotangulia kutia bao.

Atletico Madrid na Villarreal ziliendeleza mila ya Spian ya kutamba katika vikombe vya ulaya.Zote zinajiunga na ku ndi hilo la timu 32 zilizobakia bado kuania kombe la UEFA.

Kombe la dunia la klabu bingwa likikaribia kuanza ,mabingwa wa Ulaya AC Milan, wakiongozwa na stadi wao Kaka,waliwasili leo Tokyo wakiwapungia mkono mashabiki waliofika kwa wingi kuwalahki katika uwsanja wa ndege.Milan na Boca Junior ya Argentina zinajiunga katika mashindano haya ya timu 7 katika hatua yake ya nusu-finali wiki ijayo.Sepahan ya Iran inakumbana kesho na Waitakere United ya NZ kufungua dimba.

Mshindi atapapurana na Urawa reds ya Japan kunyakua haki ya kupambana na mabingwa wa ulaya AC Milan desemba 13.Finali itakua Yokohama desemba 16.

Chelsea ya Uingereza itabidi pengine kuteremka uwanjani mwishoni mwa wiki hii bila stadi wao wa Corte d’Iviore,Didier Drogba.Drogba ameumia na huenda akafanyiwa opresheni ya goti.Huenda akawa nje ya chaki ya uwanja kwa wiki 6.Kombe la Afrika la mataifa, litaanza Januari 20 hadi Februari 10.Swali ni je,atakuwsa fit kuongoza hujuma za Ivory Coast huko Ghana ?

Mwenzake wa Kameroun,Samuel Eto’o anarudi uwanjani na sasa fit kwa kombe hilo.

Bayern Munich,viongozi wa Bundesliga-Ligi ya Ujerumani, itacheza mara 2 na timu ya dimba ya olimpik ya China hapo mwakani kabla kuanza kwa michezo ya Beijing.Mpambano wa kwanza utakua Januari 12, mjini Munich na wapili utachezwa China mwishoni mwa Mei.

Benin, iliosemekana jana imeamua kumuajiri kocha wa kijerumani Farbisch,imearifu kuwa imemaliza majadiliano na kocha mfaransa Philippe Troussier, bila maafikiano.Mwezi uliopita, Benin,itakayocheza finali za kombe la Afrika huko Ghana mwezi ujao,ilimtunukia wadhifa huo mfaransa huyo ili aiongoze kwenye mashindano hayo.Troussier, ameiambia Benin hawezi kuwa nao zaidi ya miezi 3.Hii haikuiridhisha Benin.

 • Tarehe 06.12.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CYOn
 • Tarehe 06.12.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CYOn
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com