KINSHASA:Kamishna mkuu wa haki za binadamu katika UN ziarani Kongo | Habari za Ulimwengu | DW | 14.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KINSHASA:Kamishna mkuu wa haki za binadamu katika UN ziarani Kongo

Kamishna mkuu anayehusika na masuala ya haki za binadamu katika Umoja wa mataifa Louise Abour ameanza ziara yake ya siku tano nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.

Katima ziara hii kamishna Abour anatarajiwa kukutana na rais Joseph Kabila na makundi ya kutetea haki za binadamu pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali na wanadiplomasia na mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa William Swing.

Pia amepangiwa kuelekea nchini Burundi na Rwanda kutilia mkazo haja ya kuwepo amani.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com