KINSHASA: Waziri wa uchukuzi ameachishwa kazi | Habari za Ulimwengu | DW | 06.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KINSHASA: Waziri wa uchukuzi ameachishwa kazi

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo amemfukuza kazi Waziri wa Uchukuzi,Remy Henry Kuseyo kufuatia ajali ya ndege iliyotokea siku ya Alkhamisi katika mji mkuu Kinshasa.Ndege hiyo aina ya Antonov 26 ilianguka kwenye eneo lenye nyumba,muda mfupi tu baada ya kuondoka uwanja wa ndege.

Watu 50 wamepoteza maisha yao na maafisa nchini Kongo wamesema,idadi hiyo huenda ikaongezeka kwa sababu watu wengi waliopelekwa hospitali na majeraha ya moto ni mahututi.

Msemaji wa Rais Kabila amesema,waziri wa uchukuzi Kuseyo ameachishwa kazi kwa sababu hakuweza kufanya marekebisho katika sekta ya usafiri wa ndege.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com