1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

DRC

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, inayofahamika pia kama DR Congo, DRC, DROC, RDC, COngo-Kinshasa, au Congo inakutikana katika kanda ya Afrika ya Kati. Kuanzia 1971 hadi 1997 ilikuwa inajulikana kama Zaire.

DRC inapakana na Jamhuri ya Congo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan Kusini katika upande wa Kaskazini; Uganda, Rwanda, Burundi, Tanzania upande wa Mashariki; Zambia na Angola upande wa kusini na Bahari Atlantic upande wa Magharibi. Ndiyo nchi ya pili kwa ukubwa barani Afrika kieneo, ya kwanza Kusini mwa Jangwa la Sahara, na ya kumi na moja duniani. Kwa wakaazi wake milioni 75, DRC ndiyo nchi inayozungumza Kifaransa yenye wakaazi wengi zaidi, ya nne kwa kuwa na watu wengi zaidi barani Afrika na ya kumi na tisa duniani. Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Congo vilivyoanza mwaka 1996, vilihitmisha utawala wa Mobutu Sese Seko wa miaka 31 na kuiharibu nchi hiyo. Vita hivyo vilihusisha mataifa tisa ya Kiafrika, makundi kadhaa ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa na makundi 20 ya wapiganaji wenye silaha na vilisababisha vifo vya watu milioni 5.4

Onesha makala zaidi