1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongo yatangaza mripuko wa homa ya nyani

24 Aprili 2024

Jamhuri ya Kongo imetangaza mripuko wa ugonjwa wa homa ya nyani, baada ya visa 19 kuthibitishwa katika miji mitano ikiwa ni pamoja na mji mkuu Brazzaville.

https://p.dw.com/p/4f7qj
Homa ya nyani
Kirusi cha homa ya nyani iliyoripuka Jamhuriy ya KongoPicha: Isai Hernandez/imago images

Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Gilbert Mokoki amesema hakuna vifo vilivyorekodiwa kufikia sasa, lakini ametoa wito kwa umma kuchukua tahadhari, kwa kukaa mbali na wanaoshukiwa kuambukizwa homa hiyo, kuepuka kukaribiana na wanyama na kutoshika nyama za wanyamapori kwa mikono mitupu.

Jamhuri ya Kongo yaripoti visa kadhaa vya homa ya nyani, mpox

Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO) homa ya nyani iligunduliwa kwa mara ya kwanza kwa binaadamu katika nchi jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka 1970.

Dalili zake zikiwa ni pamoja na homa, maumivu na vidonda kwenye ngozi.