1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jamhuri ya Kongo yaripoti visa kadhaa vya homa ya nyani

14 Machi 2024

Jamhuri ya Kongo imerekodi visa vyake vya kwanza vya homa ya nyani au mpox katika maeneo kadhaa nchini humo.

https://p.dw.com/p/4dWsK
Homa ya nyani yaripotiwa DRC
Kirusi cha homa ya nyani iliyoripotiwa nchini KongoPicha: Isai Hernandez/imago images

Haya yamesemwa na wizara ya afya nchini humo katika ripoti iliyoichapisha jana, hiyo ikiwa ishara ya jinsi ugonjwa huo unavyoenea barani humo, tangu kisa cha kwanza cha kusambazwa kwake kupitia ngono kuthibitishwa mwaka jana.

Wanasayansi walisema kwamba kusambazwa kwa homa hiyo kupitia ngono ni jambo litakalowia vigumu kuudhibiti ugonjwa huo.

CDC-Afrika yaelezea matumaini ya kufikishwa chanjo ya Mpox, barani Afrika

Mwaka 2022 homa hiyo ilizua hofu ya kimataifa baada ya kuenea katika nchi 100 hasa kupitia ngono miongoni mwa wapenzi wa jinsia moja au wanaume wanaoshiriki ngono na wanaume na wanawake.