1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CDC:Matumaini ya kufikishwa chanjo ya Mpox, barani Afrika

16 Februari 2023

Shirika la kuudhibiti magonjwa barani Afrika, CDC-Africa limeeleza matumaini ya kufikishwa kwa chanjo za homa ya nyani barani humo katika kipindi cha wiki mbili zijazo, baada ya miezi kadhaa.

https://p.dw.com/p/4NbgI
Chinesischer Außenminister Qin Gang in Äthiopien
Picha: Fana Broadcasting Corporate

Kaimu mkurugenzi wa CDC Ahmed Ogwell amewaambia waandishi wa habari hii leo kwamba dozi hizo za Mpox zitapelekwa kwanza kwenye mataifa yenye mahitaji makubwa. Congo na Nigeria ni miongoni mwa mataifa hayo. 

Julai mwaka jana, shirika la afya ulimwenguni, WHO liliyataja maradhi hayo kuwa dharura ya kimataifa wakati kukishuhudiwa mlipuko barani Ulaya na Amerika Kaskazini, na kisha kuiomba jamii ya kimataifa kuisaidia Afrika.

Soma pia:Visa vya homa ya nyani vyaongezeka mara tatu barani Ulaya

Hata hivyo hakukua na taifa lililojitokeza kusaidia chanjo wala matibabu hata kuliposhuhudiwa ongezeko la maambukizi.

Tangu mwaka 2000, Afrika imeripoti karibu visa 1,000 hadi 2,000 vinavyodhaniwa kuwa vya homa ya nyani kila mwaka, lakini mwaka jana kuliripotiwa visa zaidi ya 3,000.