1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa. Kundi la kutetea haki za waandishi lataka mwandishi afunguliwe jela.

21 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzv

Kundi la kutetea haki za waandishi habari, waandishi wasio na mipaka RSF, leo limetoa wito wa kuachiliwa huru kwa mwandishi habari wa Congo ambaye alikamatwa miezi sita iliyopita na amesahaulika katika jela mjini Kinshasa.

Katika taarifa iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP, shirika hilo limetaka kuachiliwa huru kwa Bosange Mbaka , mwandishi anayefanyakazi na gazeti la mjini Kinshasa la mambenga.