1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI: Maafisa wa usalama wajadili harakati ya pamoja

27 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVR

Maafisa wa usalama kutoka kanda ya maziwa makuu wamekutana leo mjini Kigali, Rwanda kujadili uwezekano wa kuwa na harakati za pamoja kupambana na waasi katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Katika mkutano wa mwezi Aprili mwaka huu, maafisa kutoka Rwanda, Uganda, Congo na Burundi, walikubaliana kuwa serikali ya Kongo ipewe miezi ya kuyachakaza makundi ya waasi yaliyo katika misitu ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Msemaji wa jeshi la Rwanda, Jill Rutaremara, amesema mkutano wa mjini Kigali unatathmini ufanisi uliofikiwa na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika kupambana na makundi ya waasi nchini humo, kabla kujadili harakati za pamoja.