KHARTOUM: Mashambulio yanaendelea katika jimbo la Darfur | Habari za Ulimwengu | DW | 19.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KHARTOUM: Mashambulio yanaendelea katika jimbo la Darfur

Kamanda wa waasi katika jimbo la Darfur amesema,serikali ya Sudan imefanya mashambulio makubwa kaskazini mwa jimbo hilo,licha ya makubaliano ya kufanywa majadiliano mapya kati ya pande zote zilizohusika katika mgogoro huo. Kamanda Jar el-Neby wa kundi la waasi la NRF lililokataa kutia saini makubaliano ya amani mwezi wa Mei amesema,mapambano yaliendelea siku ya Jumamosi na Jumapili baada ya vikosi vya serikali na wanamgambo wanaojulikana kwa jina la Janjaweed,kushambulia vituo vya waasi katika eneo la Bir Mazza siku ya Jumatano na Alkhamisi.Umoja wa Afrika umethibitisha kuwa mapigano yanaendelea lakini msemaji wa majeshi ya Sudan amekanusha madai hayo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com