KHARTOUM: Kundi la waasi Darfur lakubali kuweka chini silaha | Habari za Ulimwengu | DW | 16.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KHARTOUM: Kundi la waasi Darfur lakubali kuweka chini silaha

Nchini Sudan kundi jingine la waasi katika jimbo la mgogoro la Darfur,ambalo ni moja kati ya makundi makuu matatu ya waasi,limekubali kuweka chini silaha zake.Taarifa hiyo ilitolewa na kamanda mmojawapo wa kundi hilo,baada ya kuwa na majadiliano pamoja na mjumbe wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson na mjumbe wa Umoja wa Afrika,Salim Ahmed Salim.Kutoka makundi hayo matatu ya waasi,ni kundi moja tu lililotia saini makubaliano ya amani ya mwezi Mai mwaka 2006 pamoja na serikali ya Sudan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com