Kesi ya kiongozi wa zamani wa Liberia Charles Taylor yaanza kusikilizwa | Matukio ya Kisiasa | DW | 05.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Kesi ya kiongozi wa zamani wa Liberia Charles Taylor yaanza kusikilizwa

Kesi ya kiongozi wa zamani wa Liberia Charles Taylor imeanza kusikizwa leo katika mahakama ya The Hague,huku ikivuta hisia za watu wengi na kugonga vichwa vya habari duniani.

Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor

Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor

Charles Taylor anatuhumiwa kulifadhili kundi la waasi katili la Revolutionary United Front RUF lililoendesha vita vya kikatili vya miaka 11 vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone vilivyoua maelfu ya watu.
Hata hivyo Charles Taylor mwenyewe hakufika mahakamani, na wakili wake Karim Khan aliondoka mahakamani kufuatia majibishano na jaji akisema mteja wake anaona hatatendewa haki kwa kuwa na wakili mmoja.

Aboubakary Liongo amezungumza na mkuu wa Idara ya Habari katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya mjini Freetown,Sierra Leone alikoshtakiwa mara ya kwanza Charles Taylor, Said Msonda. Kwanza alitaka kujua wananchi wa huko wanaifuatilia vipi kesi hiyo.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com