1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Liberia

Ni nchi iliyoko kwenye pwani ya Afrika Magharibi. Maana ya Liberia ni “taifa la watu huru” katika lugha ya Kilatini. Inapakana na Sierra Leon, Guinea na Cote d’ivoire.

Jamhuri ya Liberia, iliyoanza kama eneo la makaazi ya chama cha kikoloni cha Marekani (ACS) ilitangaza uhuru wake mnamo Julai 26, 1847. Marekani haikutambua uhuru wa Liberia hadi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani Februari 5, 1862. Kati ya Januari 7, 1822 na wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani, Wamarekani 15,000 wenye asili ya Afrika waliochiwa huru na waliozaliwa huru , na Waafrika wa Carribian wapatao 3,198 walihamia kwenye eneo hilo. Walowezi hao wa Kimarekani weusi walihama na utamaduni wao katika eneo hilo. Katiba na bendera ya Liberia vilitengenezwa kwa kufuata mfano wa Marekani.

Onesha makala zaidi