KATHMANDU:Jeshi la Kimao lajiondoa serikalini | Habari za Ulimwengu | DW | 19.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KATHMANDU:Jeshi la Kimao lajiondoa serikalini

Jeshi nchini Nepal limejiondoa katika serikali ya muungano na kutatiza zaidi mkwamo wa kisiasa nchini humo.Jeshi hilo lililokuwa na waasi wa zamani wanatangaza kususia uchaguzi ujao mpaka pale utawala wa kifalme utakapoondolewa kabisa.

Hata hivyo wanaonya kuandamana ifikapo Oktoba tarehe 4 hadi 6.Kundi hilo la waasi wa zamani wa Kimao limengangana kwa muda mrefu kumiliki ufalme huo wa Nepal unaokabiliwa na umasikini mkubwa kabla kujiunga rasmi na serikali baada ya Mfalme Gyanendra kulazimika kuachia madaraka yake mwaka jana. Kwa mujibu wa naibu kiongozi wa kundi la Mao Baburam Bhattarai waasi hao wanapanga kuwahusisha wafuasi wao wote kuwasilisha malalamiko yao kabla kugoma mwezi ujao.Aidha wanaonya kutumia nguvu endapo serikali itajaribu kuwasambaratisha.Kundi hilo lililazimika kuondoka serikalini kwa madai kuwa hakuna hatua yoyote iliyopigwa ili kutimiza madai yao ya kumalizwa kwa utawala wa kifalme

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com