Kasyanov azuiliwa kugombea urais wa Urusi
28 Januari 2008Matangazo
Maafisa wa tume ya uchaguzi nchini Urusi wamemzuia waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Mikhail Kasyanov, asigombee katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika tarehe mbili mwezi Machi nchini humo.
Kamati kuu ya tume ya uchaguzi ya Urusi imekataa kumsajili Kasaynov, ikisema kumegunduliwa sahihi bandia katika orodha ya wafuasi wake.
Kasyanov alikuwa waziri mkuu wa Urusi wakati wa utawala wa rais Vladamir Putin, lakini amekuwa mmoja kati ya wakosoaji wakubwa wa Urusi.
Kiongozi huyo sasa anawataka Warusi waugomee uchaguzi ujao.