KANDAHAR: Waasi 25 wa Taliban wauwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 09.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KANDAHAR: Waasi 25 wa Taliban wauwawa

Waasi takriban 25 wa Taliban wameuwawa kusini mwa Afghanistan katika visa viwili vya mapigano.

Wapiganaji watano wameuwawa na wengine wanne wakajeruhiwa wakati wa mapigano yaliyotokea katika mkoa wa Kandahar kusini mwa Afghanistan.

Duru za polisi zinasema maofisa wanne wa polisi wamejeruhiwa pia katika mapigano hayo yaliyozuka wakati genge la waasi wa Taliban walipowashambulia wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya Afghanistan waliokuwa wakifanya uchunguzi wakijiandaa kujenga barabara mpya katika wilaya ya Dand.

Wafanyakazi wawili raia wa Pakistan wametekwa nyara na waasi wa Taliban katika kisa hicho.

Wakati haya yakiarifiwa kamanda wa jeshi la NATO nchini Afghanistan, David Richards, ameonya ikiwa misaada ya kiutu haitapelekwa kwa wingi na kwa haraka nchini humo, huenda idadi kubwa ya waafghanistan wakawaunga mkono waasi wa Taliban.

´Kufikia wakati huu mwaka ujao, nitaelewa ikiwa waafghanistan wengi hususan wa eneo la kusini watatuambia, mnashindwa mwaka baada ya mwaka kutimiza ahadi zenu kwetu. Na ikiwa hamtabadili, tutaanza kusema afadhali tuongozwe na Taliban.´

Luteni jenerali David Richards amesema Afghanistan iko katika njia panda.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com