Kampuni la Arcandor sasa lafilisika ? | Masuala ya Jamii | DW | 10.06.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Kampuni la Arcandor sasa lafilisika ?

Nini hatima ya wafanyikazi wake ?

Karstadr-saa imegonga.

Karstadr-saa imegonga.

Maoni ya wahariri wa magazeti ya ujerumani hii leo takriban yote yametuwama juu ya mada moja:Kushindwa kwa juhudi za kuliokoa kampuni kubwa la Arcandor linalojumuisha duka kubwa la karstadt,Quelle na lile la utalii la Thomas Coock. Gazeti la BILD ZEITUNG (BILSAITUNG) kutoka Berlin ,laandika:

"Juhudi za kuliokoa shirika la ARCANDOR zimeshindwa na sasa linaingia katika utaratibu wa kuwa limefilisika. Ingawa kampuni hilo halikupendelea kupelekwa Mahkamani kufuqata utaratibu wa kufilisika,kwa wafanyakazi wa kampuni hilo ni kidonge kichungu kumeza.Kwani, sasa wanabidi kunywa dawa chungu waliopewa na mameneja wa kampuni lao.Mameneja walioweka ndoto ya wanunuzi wenye vitita vya fedha na kuwasahau wanunuzi wa kawaida. Matokeo yake sasa wafanyakazi 43,000 wanatapia kazi zao na mishahara yao kwa kazi zao za kujitolea kwa dhati.Hizi ni familia 43,000 na hatima yao."

Ama gazeti la SUDWEST-PRESSE kutoka Ulm linahisi kwa watumishi wa kampuni la ARCANDOR ni mstuko mkubwa kusikia kampuni lao sasa linajisajili kufilisika.Hadi dakika ya mwisho wakitumai kuwa serikali ya Ujerumani ingeingilia kuwaokoa ama kwa kulichukulia dhamana au kwa kulipa mkopo wa dharura.

Gazeti laongeza:

"Si jukumu la serikali kuyaokoa makampuni na kukiuka kanuni za mashindano ya kibiashara na hasa makampuni yaliofilisika kutokana na uongozi mbaya wsa mamaneja wake.Serikali pia imeona hayo na hivyo imekataa kusaidia.Msimamo huu iuanganie...."

Nalo gazeti la OSNABRUECKER ZEITUNG

linasema wenye kufaa kulaumiwa kwa msiba huu wa sasa ni viongozi wa juu ya kampuni hili.Gazeti laendelea:

"Mabaya zaidi wamefanya wamilikaji kampuni hili.Wao kwanza wameruhusu uongozi wa kampuni kufanya kosa moja baadae ya jengine.Kwani ikiwa sihivyo, bodi inayolisimamia ilikuwa wapi na kwanini mkondo wa mambo haukurekebishwa ?

Pili, na hii hasa kwa watumishi wake inachoma, kukaa nyuma kwa wamilikaji wa kampun i hilo ni ushahidi wa ukosefu wa imani zao katika uimara wa ARCANDOR...."

Likituhetimishia ukaguzi huu wa safu za wahariri ,gazeti la NUREMBERGER ZEITUNG (NURUNMBAGA SAITUNG) laandika:

"Kampuni hili lenye bidhaa za kila aina kuanzia A hadi Z,lilikuwa na karata mbaya tangu kabla kuanza kwa msukosuko wa sasa wa kiuchumi.Serikali ya Ujerumani kwahivyo, imefanya vyema kutoliokoa ARCANDOR kwa fedha za walipakodi.

Katika utaratibu wa kujitangaza limefilisika, kampuni hili liache maneno matupu na litende ili lichangie katika hatua hiyo kuokoa nafasi nyingi za kazi ili enzi ya kunawiri kwa shirika kubwa la bidhaa la Ujerumani chini ya uongozi wa METRO,inafufuka tena."

Mwandishi :Ramadhan Ali/ Presse /DPAE

Mhariri:M.Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com