1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeni za uchaguzi

Oumilkher Hamidou17 Agosti 2009

Joto la kampeni za uchaguzi lazidi kupanda

https://p.dw.com/p/JClE
Mtetezi na mgombea wadhifa wa kansela:Angela Merkel na Frank-Walter SteinemeierPicha: Game Group GmbH

Kampeni za uchaguzi mkuu na jinsi madawa ya kuimarisha misuli yanavyoathiri utamu wa mashindano ya riadha ni miongoni mwa mada ziliozohanikiza magazetini hii leo.

Tuanze lakini na siasa na jinsi wahariri wanavyoichambua kampeni ya uchaguzi mkuu.Gazeti la "AUGSBURGER ALLGEMEINE" linaandika:

Kampeni iliyopwaya ya uchaguzi inawafaidisha zaidi wana CDU/CSU.Kwa mujibu wa utafiti wa maoni ya umma,kansela Angela Merkel anazidi kun'gara kileleni mwa orodha ya wanasiasa wanaopendwa humu nchini.Pendekezo la vyama ndugu vya kihafidfhina kwa wapiga kura linatanguliza mbele majina mawili:Merkel na Gottenberg-majina ya wanasiasa wawili wanaoppendwa zaidi kuliko wote humu nchini.Upande wa pili ,SPD hadi wakati huu wamekua wakijaribu bila ya kufanikiwa kupalilia cheche za moto za kampeni ya uchaguzi ili kuwahamasisha wafuasi wake.Matamshi makali makali yameanza kusikika tangu mwishoni mwa wiki.Mkuu wa chama Müntefering anamkaripia Merkel huku waziri Gabriel akimshambulia Guttenberg.Wengine wanaonya dhidi ya muungano wa vyama vya rangi nyeusi na manjano.Mpaka sasa lakini yote hayo hayajasaidia kitu."

Gazeti la "BILD-ZEITUNG" la mjini Berlin linasema kampeni ya uchaguzi isingekua na tabu kama..........

"Katika kila chama watu wangetaja kile wanachopanga kukitia njiani na kwa namna hiyo kufichua kasoro zilizoko upande wa pili.Hapo tena wapiga kura watachagua mpango gani wanauona ndio bora.SPD wamejaribu .Kwa kuchapisha "mpango kwa Ujerumani",SPD wametoa mkakati ambao unastahiki kujadiliwa.Lakini CDU/CSU wanapinga kuingia katika mjadala kama huo.Sasa kiongozi wa SPD nae Franz Münterfering anapalilia mambo:sio kwa kutoa mapendekezo ziada,bali kwa dhana zake eti idadi ya wasiokua na ajira haimshughulishi hata kidogo Angela Merkel .Wana CDU wamejibu.Hata kama kampeni ya uchaguzi imechangamka,lakini wapiga kura wao hawavutiwi na malumbano kama hayo.Matokeo yake,siku ya siku inapowadia,wanaona bora kusalia nyumbani badala ya kuteremka vituoni."

Sport Leichtathletik WM Berlin Deutschland 100m Flash-Galerie
Mashindano ya kimataifa ya riadha mjini BerlinPicha: AP

Mada yetu ya mwisho magazetini inahusu michezo.Wahariri wanasikitika na kusema kokote kule ambako wanariadha wanakutana na kujaribu kupimana nguvu,dhana haikosekani,pengine wamemeza madawa ya kuimarisha misuli.Gazeti la "Die WELT " la mjini Berlin linaandika:

Kusema kweli,michezo kwa jumla,ikichanganyika pia michuano ya riadha,imepoteza hadhi yake kutokana na visa visivyokwisha vya madawa ya kulevya.Hivi sasa watu wanafyetuka mabio,wanavurumisha au hata wana ruka na kuchupa,wakifuatana na dhana jumla ya kutumia madawa ya kuimarisha misuli.Hata wanaspoti wenyewe kwa wenyewe,hawaaminiani.Dhana zinagubika michuano mfano mwa hii ya kimataifa inayoendelea katika uwanja wa Olympik mjini Berlin.

Gazeti la TAGESSPIEGEL linahisi:

Hakuna kama kuwepo kiwanjani.Mashindano ya riadha yanasisimua kutokana na fani zake mbali mbali.Lakini yamepoteza sifa iliyokua nayo ya kutia fora.

Kwa maoni hayo ya TAGESPIEGEL kutoka Berlin ndio na sisi tunazifunga kurasa za magazeti ya Ujerumani kutoka Deutsche-Welle mjini Bonn.............

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Othman MIraji