KABUL:Serikali yakubali kuukabidhi mwili wa Mullah | Habari za Ulimwengu | DW | 05.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL:Serikali yakubali kuukabidhi mwili wa Mullah

Serikali ya Afghanistan imekubali kuukabidhi mwili wa kamanda wa kundi la Taliba kwa familia yake, kwa kubadilishana na wafanyakati watano wa afya wanaoshikiliwa mateka na wanamgambo wa kundi hilo.

Maafisa wa Serikali wamesema kuwa wafanyakazi hao walitekwa nyara mwezi march mwaka huu katika jimbo la kusini la Kandahar.

Watekaji nyara hao walikuwa wakidai kuachiwa kwa wafungwa wa kitaliban, lakini wiki hii wakabadilisha msimamo na kusema kuwa wanataka kubadilishana na mwili wa kamanda wa kundi la Taliban Mullah Dadullah ambaye aliuawa na majeshi ya Marekani mwezi uliyopita.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com