KABUL: Wanajeshi sita wa Canada wauwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 09.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Wanajeshi sita wa Canada wauwawa

Wanajeshi sita wa Canada waliuwawa jana na wengine wawili kujeruhiwa kusini mwa Afghanistan wakati gari walimokuwa wakisafiria lilipolipuwa na bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara.

Shambulio hilo limeelezwa kuwa baya zaidi kuwahi kufanywa dhidi ya wanajeshi elfu 33 wa jeshi la muungano linaloongozwa na shirika la kujihami la kambi ya magharibi, NATO, linalokabiliana na wanamgambo wa kundi la Taliban nchini Afghanistan.

Wizara ya ulinzi nchini Canada imetangaza kwamba tukio hilo lilitokea magharibi mwa Kandahar, ngome ya waasi wa Taliban.

Katika tukio lengine mwanajeshi mmoja wa NATO aliuwawa na mwengine kujeruhiwa kwenye shambulio la bomu kusini mwa Afghanistan.

Msemaji wa jeshi la NATO amethibitisha habari hizo lakini hakusema ni wapi shambulio hilo lilikotokea.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com