KABUL: Shambulio la wanamgambo limeua watoto 2 | Habari za Ulimwengu | DW | 20.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Shambulio la wanamgambo limeua watoto 2

KABUL:

Shambulio la kujitolea muhanga lililofanywa dhidi ya vikosi vya NATO kusini mwa Afghanistan limeua si chini ya watoto 2.Mwanajeshi mmoja wa Kingereza aliuawa katika shambulio hilo na watu 10 wengine walijeruhiwa ikiwa ni pamoja na wanajeshi 2 wa Kingereza.Mshambuliaji alijipeleka karibu na kikosi cha Kingereza katika mji mkuu Lashkar Gah wa wilaya ya Helmand,ambayo ni ngóme ya Wataliban.Katika shambulio jingine la bomu la kujitolea muhanga kwenye wilaya ya mashariki ya Khost,afisa mmoja wa polisi aliuawa baada ya mshambuliaji kujirusha mbele ya gari ya doria.Maafisa wengine watano walijeruhiwa katika mripuko huo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com