Kabul . Ndege za Tonado zaenda Afghanistan. | Habari za Ulimwengu | DW | 05.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kabul . Ndege za Tonado zaenda Afghanistan.

Ndege sita za kivita kutoka Ujerumani chapa Tonado zilizotumwa kusaidia majeshi ya NATO nchini Afghanistan zimewasili katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mazar-e-Shariff.

Ndege hizo sita zinatarajiwa kuingizwa katika utaratibu wa jeshi la NATO siku ya Jumatatu na kuanza kazi za upelelezi katika anga la kusini mwa Afghanistan hapo Aprili 15.

Ndege hizo zitakusanya taarifa kwa ajili ya jeshi la ardhini la NATO linalopigana na mabaki ya utawala ulioondolewa madarakani wa taliban.

Bunge la Ujerumani limekubali kuwekwa kwa ndege hizo nchini Afghanistan mwezi uliopita.

Ndege hizo zitahudumiwa na wanajeshi 200.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com