Jumuiya ya kimataifa yatakaa kutambua ushindi wa Gbagbo
4 Desemba 2010Jumuiya ya kimataifa inakataa kumtambua mshindi aliyetangazwa katika uchaguzi mkuu wa rais nchini Ivory Coast Laurent Gbagbo. Umoja wa Ulaya, umoja wa mataifa , pamoja na Ufaransa na Marekani zinamtambua Alassane Ouattara kuwa ndie mshindi wa uchaguzi huo. Jana Ijumaa , baraza la katiba la Ivory Coast lilibadilisha matokeo ya uchaguzi huo ambayo yameonyesha kuwa Ouattara amepata zaidi ya asilimia 54 ya kura. Wanaowaunga mkono wagombea wote wawili wameingia mitaani kuonyesha uungaji wao mkono na hofu ya kutokea ghasia bado ipo juu baada ya watu 15 kuuwawa baada ya uchaguzi huo. Jeshi limefunga mipaka ya nchi hiyo ya Afrika magharibi na matangazo ya vyombo vya habari vya kigeni yamezuiwa. Rais Laurent Gbagbo anatarajiwa kuapishwa hii leo Jumamosi.