JOHANNESBURG : Kansela Merkel awasili Afrika Kusini | Habari za Ulimwengu | DW | 05.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JOHANNESBURG : Kansela Merkel awasili Afrika Kusini

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amewasili nchini Afrika Kusini jana usiku kwa ziara ya siku mbili ambapo anategemewa kuishinikiza serikali ya nchi hiyo juu ya suala la Zimbabwe.

Merkel ambaye jana alianza ziara yake ya kwanza kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika kwa wito wa kuwepo kwa demokrasia zaidi nchini Ethiopia anatazamiwa kukutana na Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini leo asubuhi mjini Pretoria.

Baadae anatazamiwa kutembelea eneo kunakojengwa uwanja wa mpira ambao utachezesha fainali za michuano ya soka kombe la dunia hapo mwaka 2010.

Hapo kesho Merkel anatarajiwa kukutana na rais mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela na kutembelea miradi ya kupiga vita UKIMWI na ile ya mazingira mjini Cape Town.

Hapo Jumapili kiongozi huyo wa Ujerumani ataizuru Liberia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com