Jeshi la Marekani laanzisha oparesheni Afghanistan. | Matukio ya Kisiasa | DW | 02.07.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Jeshi la Marekani laanzisha oparesheni Afghanistan.

Opareshi hiyo inayoendeshwa katika mkoa wa Helmand ina lengo la kuwafurusha wanamgambo wa Taliban.

default

Wanajeshi wa Marekani katika mkoa wa Helmand nchini Afghanistan.

Maelfu ya wanajeshi wa Marekani walifanya mashambulizi ndani ya ngome ya wanamgambo wa Taliban katika bonde la Helmand nchini Afghanistan mapema hii leo, ukiwa ndio mwanzo wa oparesheni mpya ambayo Marekani inaamini kuwa itabadili vita nchini Afghanistan.

Oparesheni hii ndio ya kwanza na kuu ambayo pia ni moja ya harakati mpya za Marekani nchini Afghanistan inayowajumuisha wanajeshi 8,500 waliowasili katika mkoa huo ulio kusini mwa Afghanistan mwezi miwili iliyopita, kujiunga na wanajeshi wa Uingereza walioko katika ngome za kundi la Taliban nchini Afghanistan.

Wanajeshi hao wa Marekani ndicho kikosi kubwa zaidi kati ya wanajeshi 17,000 na wengine 4000 wataowapa mafunzo wanajeshi wa Afghanistan, kufika nchini Afghanistan kutokana na amri iliyotolewa na rais wa Marekani Barack Obama.

Idadi ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan itafikia wanajeshi 68,000 itimiapo mwishoni mwa mwaka huu, mara mbili zaidi ya wanajeshi 32,000 waliokuwa nchini Afghanistan hadi mwishoni mwa mwaka uliopita.

Mkoa wa Helmand ndio mkoa mkubwa zaidi nchini Afghanistan. Wanajeshi hao wa Marekani wanajiunga na wanajeshi 9000 wa uingereza ambao wamekuwa nchini Afghanistan tangu mwaka 2006.

Wanajeshi kutoka Canada , Uholanzi na wengine kutoka shirika la kujihami la nchi za magharibi NATO wamaekuwa wakishirikiana na wanajeshi wa Uingereza katika mapigano kwenye mkoa wa Helmand katika opareshini iliyotajwa mwaka uliopita na makamanda wa Marekani kuwa iliyokwama.

Wanajeshi waliokuwa wakiendesha opareshi hiyo hawakuweza kukabiliana na ukubwa pamoja na na hali ngumu ya eneo hilo kijiografia, iliyo na jangwa kubwa eneo la kusini na milima katika eneo la kaskazini.Naibu kamanda wa jeshi la NATO kusini mwa Afghanistan ameonya kuwa huenda kukawa na umwagaji mkubwa wa damu.

Wakazi wengi katika mkoa wa Helmand wanatoka katika kabila la Pashtun kabila kubwa zaidi nchini Afghanistan na wamekuwa wakioongoza nchi hiyo. Mkoa wa Helmand unapaka na eneo la kusini mwa Pakistan.

Maafisa wanasema kuwa wilaya nne kati ya wilaya 13 katika mkoa wa Helmand, zinadhibitiwa na kundi la kundi la Taliban. Helmand pia unazalisha zaidi ya nusu ya bangi nchini Afghanistan ambayo pia inazalisha karibu asilimia 90 ya bangi duniani

Aliyekuwa kamanda la jeshi hilo jnerali Stanely McChrystal sasa anaongoza kikosi cha wanajeshi 90,000 kinacho wajumuisha wanajeshi wa Marekani pamoja na wale kutoka NATO.

Luteni jenerali David Rodriguez anachukua uongozi wa shughuli za kila siku za vikosi vya kigeni nchini Afghanistan. Mbinu zinazotumiwa na jeshi hili ni sawa na alizotumia jenerali David Petraeus nchini Iraq ambaye sasa ni kamanda wa vikosi vya Marekani katika ASia ya kati pamoja na mashariki ya kati.

Mtangulizi wa jenerali McChrystal jenerali David McKiernan aliondolewa baada ya kushindwa kukabiliana na kuongezea kwa ghasia nchini Afghanisatan.

Jenerali McChrystal anasema kuwa mikakati yake ni kuwatenganisha wanamgambo na raia wa kawaida akisema wanajeshi wa kigeni wanahitajika kuwashawishi raia kuwaua wanamgambo hao

Mwandishi :Jason Nyakundi/RTRE

Mhariri :Mohamed Abdul Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com