Jeshi la Israel laingia Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 04.01.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Jeshi la Israel laingia Gaza

Mapigano makali yaripotiwa na maisha yaangamia


 Israel inaendelea kuhujumu Gaza,kupitia vikosi vya nchi kavu ,angani na baharini.Vyomo vya habari vinazungumzia juu ya wapalastina kadhaa waliopoteza maisha yao kutokana na hujuma hizo.Havikutaja lakini idadi ya wahanga hao.Duru za kuaminika zinazungumzia juu ya wapalastina zaidi ya 19 waliouwawa pamoja pia nna askari jeshi mmoja wa Israel.Jeshi la Israel linazungumzia juu ya majeruhi 30 kati ya wanajeshi wake kufuatia mapambano makali dhidi ya wanamgambo wa Hamas.Kwa mujibu wa ripoti za kituo kimoja cha matangazo cha kiarabu,vifaru vya Israel vimeshaingia katika mji mkuu wa Gaza hivi sasa.Wafuasi wa itikadi kali ya dini ya kiislam Hamas wamesema wamemkamata mwanajeshi mmoja wa Israel.Israel inasema wanajeshi wake wamepania kuteketeza mahala makombora ya Hamas yanakofyetuliwa.Hata hivyo makombora ya Kassam na maguruneti yamevurumishwa  tena hii leo dhidi ya Israel.Jeshi la Israel limewataka maelfu ya wanajeshi waakiba warejee jeshini.

 • Tarehe 04.01.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GRjO
 • Tarehe 04.01.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GRjO
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com