Jeshi la bara la Afrika kufunzwa nchini Ujerumani. | Matukio ya Kisiasa | DW | 08.06.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Jeshi la bara la Afrika kufunzwa nchini Ujerumani.

Bila usalama hakuna maendeleo katika bara la Afrika ndivyo anavyosema mkuu wa idara ya kiraia ya jeshi la AFRICOM balozi Ary Carvin Yates.

Bila ya usalama hakuna maendeleo katika bara la Afrika, hii inajionesha katika mizozo kadha katika bara hilo.

Bara hilo limeingia katika ajenda ya usalama nchini Marekani. Limeundwa kundi la wanajeshi la AFRICOM , Oktoba 2007 likiwa na makao yake makuu mjini Stuttgart. Mataifa ya Afrika ni lazima yatayarishe majeshi yao kwa kupata mafunzo ili kujiendeleza.

AFRICOM litakuwa ni sehemu ya kusikiliza.Ni kutokana na kitu ambacho mataifa ya Kiafrika yalikihitaji. Ama kwa upande wa sekta ya kiraia muhusika atakua Balozi Ary Carvin Yates. Ute Schaeffer ameandika yafuatayo na msimulizi ni Sekione KitojoHadi sasa kunapatikana katika bara la Afrika mabaki ya vita baridi. Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Angola, Msumbiji, Sierra Leone na Liberia ni matokeo yake. Baada ya kuvunjika kwa kambi za mashariki na magharibi baadhi ya mataifa ya Afrika yalibaki bila ya utaratibu wa kisiasa na bila ya uzoefu wa kuendesha serikali kupitia bunge. Kama hiyo haitoshi, hali mbaya ya kiusalama ililikabili bara hilo. Mataifa yaliyoko katika jangwa la Sahara, na hata mataifa ya Afrika mashariki yakawa maeneo ya maficho ya makundi ya kigaidi ya Kiislamu.

Kutokana na vita pamoja na yale mataifa yanayoonekana kuwa yaliyoshindikana kuna kuwapo na hatari kubwa, na Somalia ni mfano halisi.

Tangu Oktoba 2007 Marekani ndio sababu ilijaribu kufanikisha kuwapo kikosi hiki cha jeshi kwa ajili ya bara la Afrika. AFRICOM Limechukua operesheni zote zilizokuwa zinafanywa na majeshi ya Marekani katika eneo lote la bara la Afrika ukiiondoa Misr tu.

Kuwapo na uwakilishi katika pande zote kwa jeshi hilo kama balozi Mary Carlin Yates anavyosisitiza , ni nani ataweza kuwa mkuu wa kijeshi badala ya generali William Kip Wards.

Anaongoza kazi za kiraia za AFRICOM na kusisitiza kuwa AFRICOM inafuata siasa za D tatu kubwa.

Ulinzi, diplomasia na maendeleo, ndio yaliyosababisha kujenga jeshi hili. Kwa nadharia hiyo, lakini hili ni jeshi, kwa hiyo nguzo nyingine mbili za kiti hiki, ni nguzo ambazo tunaziunga mkono ama kuchukua mwelekeo wa ishara ya kidiplomasia.Akiwa balozi wa zamani nchini Ghana Yates anafahamu bara hili vizuri. Hivi karibuni atakuwa mjini Washington afisa mwandamizi wa rais Obama.

Kwake yeye mapambano dhidi ya umasikini ni kufanikisha kuwapo usalama zaidi kwa Afrika.

Mapambano ya umasikini, elimu, afya, miundo mbinu , haya yote ni misingi ya usalama na uthabiti ambayo watu wa Afrika wanahitaji, na nafikiri ndio wizara ya mambo ya nje na serikali ya Marekani imekuwa ikifanyia kazi kwa muda mrefu. Kile ambacho mpango wa kijeshi unafanya kuhusiana na ushirikiano wa kiusalama ni kutafuta njia za kusaidia mipango inayoendelea na wana mipango ya kijeshi yao wenyewe.

Na mataifa tisa ya jangwa la Sahara yameandaa luteka ya pamoja ya jeshi la AFRICOM ili kuweza kupambana na ugaidi.

Hapa pia kwa mataifa washirika katika bara la Afrika imeongezeka hali ya kujiamini.

►◄

Mwandishi:Ute Schaeffer/Afrika Nahost/Sekione Kitojo

Mhariri:M.AbdulRahaman • Tarehe 08.06.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/I5nV
 • Tarehe 08.06.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/I5nV
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com