JERUSALEM: Ndege za Kiisraeli zimeshambulia Ukanda wa Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 16.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM: Ndege za Kiisraeli zimeshambulia Ukanda wa Gaza

Vikosi vya anga vya Israel vimefanya mashambulio katika Ukanda wa Gaza,vikilenga nyumba za wanamgambo wa Kipalestina.Hakuna ripoti kuhusu hasara ya maisha iliyosababishwa na mashambulio hayo.Mashahidi wanasema,kabla ya kufanya mashambulio,jeshi la Israel liliwaonya wenye nyumba watoke nje.Mashambulio hayo yamefuatia shambulio la roketi lililofanywa na wanamgambo wa Kipalestina kutoka Gaza.Shambulio hilo lililolenga mji wa Kiisraeli wa Sderot,limemuuawa mwanamke mmoja na wengine watano wamejeruhiwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com