JERUSALEM: Israel yapanga shambulio kubwa kwenye ukanda wa Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 23.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM: Israel yapanga shambulio kubwa kwenye ukanda wa Gaza

Serikali ya Israel imechukuwa hatua ya kufanya mashambulizi zaidi ya ndege na mauaji ya kuvizia kwenye ukanda wa Gaza kukomesha kile imekitaja mashambulizi ya makombora kwenye miji ya Israel. Lakini serikali imesema haijaruhusu uvamizi.

Taarifa ya serikali imesema, majeshi ya usalama yameamrishwa kutayarisha mpango wa operesheni kubwa. Masaa machache baada ya tamko hilo, vifaru na magari ya kijeshi zaidi ya Israel yameonekana yakiingia kwenye ukanda wa Gaza kuwakuta wanajeshi wengine wanaokuwa huko. Duru kutoka Hospitali kwenye ukanda wa Gaza, zimesema wanajeshi wa Israel wamawauwa wapiganaji wawili wa chama tawala cha Hamas.

Kwa upande mwingine, raia moja ambaye alijeruhiwa na kombora la wapalestina kwenye mji wa Sderot amefariki dunia kutokana na majeraha.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com