JERUSALEM: Israel yamteua kiongozi mpya wa jeshi | Habari za Ulimwengu | DW | 23.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM: Israel yamteua kiongozi mpya wa jeshi

Israel imemtaja meja jenarali Gabi Ashkenazi kuwa kiongozi mpya wa jeshi, kufuatia kujiuzuzulu kwa luteni jenerali Dan Halutz wiki iliyopita.

Jenerali Ashkenazi mwenye umri wa miaka 52 ni mwanajeshi ambaye hivi sasa ni mkurugenzi mtendaji wa wizara ya ulinzi. Jenerali Halutz alijiuzulu baada ya kukosolewa vikali kwa jinsi alivyoviendesha vita kati ya Israel na kundi la Hezbolla mwaka jana.

Haijabainika wazi ikiwa jenerali Ashkenazi atachukua wadhifa wake mpya, kwani uteuzi wake lazima uidhinsihwe na bunge na kamati ya utumishi wa serikali.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com