Jaribio la kigaidi: Marekani | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 26.12.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Jaribio la kigaidi: Marekani

Raia mmoja wa Ki-Nigeria amekamatwa kufuatia jaribio la kuilipua ndege moja ya Marekani.

Ndege ya shirika la ndele la Northwest 253 ilipowasili, katika uwanja wa ndege wa Detroit kutoka Amsterdam.

Ndege ya shirika la ndele la Northwest 253 ilipowasili, katika uwanja wa ndege wa Detroit kutoka Amsterdam.

Rais Barack Obama ameagiza kuchukuliwa hatua za ziada za kiusalama katika usafiri wa ndege, baada ya mtu mmoja kujaribu kulipua ndege moja ya shirika la Marekani iliyokuwa inaelekea Detroit kutoka mjini Amsterdam. Mtu huyo ambaye anasemekana ni raia wa Nigeria, alikuwa abiria ndani ya ndege hiyo, yenye chapa AIRBUS 330 iliyokuwa imewabeba abiria 278, alizidiwa nguvu na wenzake alipojaribu kuwasha fataki wakati ndege hiyo ilikuwa inatua katika uwanja wa ndege huko Detroit. Vyombo vya habari vya Marekani, vinaripoti kuwa mtu huyo amewaambia maafisa wa usalama kuwa alitoa fataki hizo na maagizo ya kuilipua ndege hiyo kutoka nchini Yemen. Rais Obama ambaye yuko likizoni huko Haiwaii anasemekana anafuatilia matukio, lakini hajabadili ratiba yake. Taarifa kutoka shirika la ndege la Northwest zinasema raia huyo wa Nigeria amekamatwa na abiria wengine walihojiwa kufuatia tukio hilo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com