JAKARTA: Tetemeko jipya la ardhi Indonesia
13 Septemba 2007Matangazo
Tetemeko jingine kubwa la ardhi limetokea mapema leo asubuhi katika kisiwa cha Sumatra nchini Indonesia.Tetemeko hilo lilikuwa na nguvu ya 7.8 katika Kipimo cha Richter.Saa chache kabla ya hapo,tetemeko kubwa lililotokea katika eneo hilo,liliua hadi watu 9 na kujeruhi wengi wengine na vile vile majengo mengi yaliporomoka.