1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Italia: Maambukizi ya virusi vya coronaa yapungua kidogo

Zainab Aziz
6 Aprili 2020

Katika baadhi ya nchi za Ulaya maaambukizi ya virusi vya corona yamepungua kidogo. Nchini Ujerumani maambukizi yapindukia watu laki moja.

https://p.dw.com/p/3aUCQ
Coronavirus in Italien Temperatur-Messung
Picha: picture-alliance/abaca/Ipa/A. di Vincenzo

Ufaransa, Italia na Uhispania zimeripori idadi ndogo ya vifo vilivyosababishwa na virusi vya corona kwa mara ya kwanza katika muda wa wiki mbili. Nchini Italia maafisa wameanza kuzingatia hatua ya pili ya juhudi za kupambana na maambukizi mara baada ya hatua ya karantini iliyowekwa mwezi uliopita kuanza kulegezwa.

Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa homa ya mapafu, COVID-19 duniani kote imefikia watu1,272,737, watu waliokufa ni 69,418 na waliopona baada ya kutibiwa ni 261,485. Nchini Ujerumani pekee walioambukizwa wamevuka laki moja.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris JohnsonPicha: Imago Images/xi.Images/A. Parsons

Na habari kutoka Uingereza zinasema Waziri Mkuu wa nchi hiyo Boris Johnson amelazwa hospitali kwa ajili ya kufanyiwa vipimo, kutokana na kuendelea kuwa na dalili za virusi vya corona siku kumi baada ya kugundulika kuwa na maambukizi.

Chanzo:DW