1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Silvio Berlusconi

Silvio Berlusconi ni mmiliki wa vyombo vya habari na mwanasiasa wa Italia. Waziri mkuu huyo mara tatu wa Italia, amekumbwa na kashfa kadhaa katika maisha yake ya kikakazi.

Silvio Berlusconi, aliezaliwa mjini Milani mwaka 1936, alipanda kutoka tabaka la kati na kuwa mmoja wa matajiri wakubwa zaidi nchini Italia. Alizindua kituo chake cha Televisheni mwaka 1974 kabla ya kujitosa katika ulingo la siasa mwaka 1993. Alianzisha chama cha siasa mrengo wa kulia cha Forza Italia na kuhudumu mara tatu kama waziri mkuu (1994-5; 2001-6; na 2008-11). Amekumbwa na kashfa kadhaa za ngono na rushwa katika safari yake ya maisha ya kikazi. Mwaka 2013, alitiwa hatiani kuhusiana na udanganyifu wa kodi na kuzuwiwa kuwania tena uongozi. Huu ni mkusanyiko wa mada za DW kuhusu Silvio Berlusconi.

Onesha makala zaidi