Israel yazidi kushambulia wa Hamas Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 24.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Israel yazidi kushambulia wa Hamas Gaza

GAZA:

Ndege za kijeshi za Israel zimefanya mashambulizi katika ukanda wa Gaza na kuwauwa wapiganaji wa wili wa Hamas.

Msemaji wa jeshi la Israel amehakikisha shambulio hilo na kuongeza kuwa watu waliokuwa na silaha walisogelea ukuta unaotenganisha Gaza na Israel,na kuzusha wasiwasi kuwa huenda walikuwa wanapanga kushambulia vikosi vya Israel vilivyokuwa hapo karibu.

Na akizungumza hapo awali Waziri mkuu wa Israel Bw Olmert alisema hujuma dhidi ya makundi ya kigaidi zitaendelea.

Wapiganaji wa Kipalestina zaidi ya 20 wameuawa na hujuma za Israel katika eneo la Gaza katika wiki iliopita.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com